Jamhuri ya Kiislamu ya Iran imetuma shehena ya misaada ya kibinadamu kwa wakimbizi wa Kiislamu nchini Myanmar baada ya kurejea hali ya utulivu kwa kiasi fulani.Taarifa zinasema kuwa, misaada hiyo ilipitishiwa nchini Bangladesh ambayo inapakana na Myanmar baada ya nchi hiyo kugubikwa na machafuko yaliyosababishwa na Mabudha wenye misimamo mikali kuwashambulia na kuwauwa Waislamu wa jamii ya Rohingya. Waislamu hao wamewekwa katika kambi kwenye eneo la mpakani kati ya nchi hiyo na Bangladesh kwa kuhofia usalama wao.
Maelfu ya Waislamu wa Myanmar wameuawa kinyama katika mashambulizi yanayoendela kufanywa na mabudha wenye misimamo mikali kwenye vijiji na maeneo ya Waislamu nchini humo.Inafaa kuashiria hapa kuwa, asilimia sita kati ya jumla ya watu milioni sitini wa Myanmar ni Waislamu, lakini serikali ya nchi hiyo haiwatambui rasmi kama raia wa nchi hiyo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO