Sunday, January 13, 2013

ISRAEL YAWAFUKUZA WAPALESTINA WANAOPINGA VITONGOJI

Jeshi la utawala wa Kizayuni wa Israel limewaondoa kwa nguvu wanaharakati wa Palestina na wa nchi za kigeni waliokuwa wameweka mahema katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan kupinga ujenzi wa vitongoji vipya vya walowezi wa Kizayuni kwenye eneo hilo. Vikosi vya Israel vimekabiliana na kuwaondoa kwa nguvu wanaharakati karibu 200 kwenye mahema hayo. Mustafa Barghouthi Mbunge wa Palestina amesema, mamia ya askari wa Israel walizingira mahema hayo kutoka kila upande na kuwaondoa kwa nguvu wanaharakati hao ambapo wanaharakati wasiopungua 6 wamejeruhiwa. Mwezi uliopita Israel ilitangaza kuendelea na mpango wake wa kujenga nyumba mpya 6,500 katika maeneo ya Wapalestina licha ya suala hilo kupingwa na Umoja wa Mataifa, jamii ya kimataifa na Wapalestina wenyewe.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO