Sunday, January 13, 2013

MAJESHI YA UFARANSA YAUA WATU 100 MALI

Afisa wa ngazi za juu wa Mali amesema kuwa zaidi ya watu 100 wameuawa katika mashambulizi ya vikosi vya Ufaransa nchini Mali. Hii ni katika hali ambayo Rais Francis Hollande wa Ufaransa ameamuru kuimarishwa usalama katika majengo na ofisi za Ufaransa baada ya nchi hiyo kufanya operesheni nchini Mali na Somalia. Hayo yanajiri huku Uingereza ikikubali kuisaida Ufaransa kusafirisha askari na vifaa nchini Mali. Ijapokuwa Ufaransa ilidai huko nyuma kwamba haingejiingiza katika mgogoro wa Mali lakini siku ya Ijumaa ilianzisha operesheni za kuwashambulia waasi wa Mali. Rais wa Ufaransa amedai kwamba, lengo la operesheni hizo za Paris nchini Mali ni kuunga mkono kupelekewa vikosi vya nchi za Kiafrika kwenye nchi hiyo, suala ambalo limepitishwa na Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO