Waziri Mkuu wa Libya Ali Zidan amesema kuwa, viongozi wapya wa Tripoli kamwe hawatoruhusu nchi hiyo kugeuzwa kuwa uwanja wa shughuli za kigaidi na biashara haramu ya silaha. Waziri Mkuu huyo amesema hayo katika mkutano na waandishi habari pamoja na wenzake wa Tunisia na Algeria pambizoni mwa kikao cha kujadili usalama wa mipaka ya pamoja kilichofanyika katika mji wa Ghadames wa Libya. Zidan ameongeza kuwa, hali ya Mali imewalazimu wakutane ili kuchukua hatua za kuimarisha usalama wa mipaka yao na kuzuia athari za mgogoro wa nchi hiyo kwenye nchi zao. Kikao hicho cha kujadilia usalama wa mipakani kilifanywa na Mawaziri Wakuu wa Libya, Tunisia na Algeria kwa lengo la kujadili namna ya kuimarisha usalama katika mipaka ya pamoja na kukabiliana na ugaidi pamoja na wahajiri haramu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO