Saturday, January 05, 2013

HASIRA MPYA ZAZUKA KESI YA UBAKAJI INDIA


Madai ya uzembe wa jeshi la polisi nchini India yaliyotolewa na rafiki wa kiume wa msichana aliyefariki baada ya kubakwa yamezusha hasira mpya kwenye kesi ya ubakaji inayowakabili watu watano New Delhi. Hasira hizo zimezuka baada ya kijana huyo ambaye ndiye shahidi pekee wa tukio la ubakaji lililohusisha wanaume sita dhidi ya rafiki yake wa kike kueleza kwa mara ya kwanza namna rafiki yake huyo alivyobakwa.
Raia nchini India wanataka polisi iwajibike kwa tuhuma hizo. Jeshi la polisi nchini India limefungua kesi dhidi ya kituo cha televisheni cha Zee News, kutokana na kurusha mahojiano ya kijana huyo likisema kuwa kimekiuka sheria na kumuanika shahidi wa kesi hiyo nyeti. Mahojiano hayo yalimwonyesha kijana huyo bila kuficha uso wake.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO