Vikosi vya Kiitelijinsia vya Lebanon vimemtia
mbaroni raia mmoja wa nchi hiyo kwa tuhuma za kushirikiana na shirika la ujasusi
la Israel (Mossad) kwa zaidi ya miongo miwili. Mtu huyo aliyetambuliwa kwa jina
la Ali Taufiq Yari anadaiwa kuwa alilipwa na Israel dola za Kimarekani laki sita
kwa kuupatia utawala huo taarifa za siri kuhusu harakati ya Muqawama ya Lebanon
Hizbullah na jeshi la nchi hiyo. Imeelezwa kuwa mwakilishi huyo wa zamani wa
baraza la mji huko Baalbek aliwapatia maafisa wa ujasusi wa Israel taarifa
nyingi muhimu wakati wa vita vilivyoanzishwa na utawala huo wa Kizayuni dhidi ya
Lebanon mwaka 2006.
Yari ambaye imeelezwa kuwa alijiunga na Mossad
mwaka 1990 ametajwa na maafisa wa Lebanon kuwa jasusi anayelipwa kitita kikubwa
cha fedha kuwahi kutiwa mbaroni hadi sasa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO