Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia Sergei Lavrov ameonya kuwa hujuma yoyote ya
kijeshi dhidi ya Iran itasababisha maafa makubwa. Akizungumza na waandishi habari mjini Moscow, Lavrov amesema kutatua kadhia
ya nyuklia ya Iran kupitia nguvu za kijeshi ni jambo ambalo litasababisha maafa
makubwa duniani.
Katika miaka ya hivi karibuni Marekani, Utawala wa Kizayuni na waitifaki wao
wamekuwa wakitoa vitisho vya kuishambulia Iran kijeshi kwa sababu ya miradi yake
ya kuzalisha nishati ya nyuklia. Iran imesisitiza kuwa shughuli zake za nyuklia
zinafanyika kwa malengo ya amani katika fremu ya sheria za kimataifa. Kwingineko katika matamshi yake, Waziri wa Mambo ya Nje wa Russia amesema
Iran ina nafasi muhimu sana katika kutatua matatizo ya Mashariki ya kati. Lavrov
amesisitiza kuwa bila kuhusishwa Iran, matatizo mengi ya eneo hilo hayawezi
kutatuliwa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO