Thursday, January 03, 2013

OIC KUJADILI CHUKI DHIDI YA WAISLAM


Msemaji wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu (OIC) imesema kuwa, itajadili nja za kukabiliana na vitendo vya chuki dhidi ya Uislamu. Ridhwan Sheikh amesisitiza kuwa, jumuiya hiyo itafanya mkutano tarehe 7 mwezi huu wa Januari mjini Istanbul kwa lengo la kutafuta mikakati ya kukabiliana na njama za kuufanya Uislamu na Waislamu waogopwe na kuchukiwa.
Ameongeza kuwa, mkutano huo utahudhuriwa na wataalamu mbalimbali wakiwemo wanasheria na wawakilishi wa nchi za Kiislamu katika Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa na mwakilishi maalaumu wa Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu anayeshughulikia masuala yakupambana na njama za kufanya Uislamu uogopwe.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO