Wednesday, January 09, 2013

RAIS WA GAMBIA AZITUHUMU NCHI ZA UMOJA WA ULAYA

Rais Yahya Jammeh wa Gambia amezituhumu nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya kuwa zinafanya kila ziwezalo ili kuyumbisha uthabiti wa nchi hiyo. Umoja wa Ulaya umemtaka Rais Jammeh kuheshimu haki za binadamu. Rais wa Gambia amesema kuwa nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekusudia kuvuruga amani na kuasisi serikali kibaraka nchini humo ambayo itazipatia nchi hizo maliasili za nchi hiyo kwa kuwa nchi za Ulaya zinatambua vyema kuwa Gambia hivi sasa ina mafuta. Rais Yahya Jammeh wa Gambia ameyasema hayo jana jioni katika mkutano wa dharura wa serikali yake kabla ya nchi hiyo kufanya mkutano na Umoja wa Ulaya Ijumaa hii katika mji mkuu Banjul. Kufutwa hukumu ya kifo, kuyaruhusu kuanza kazi magazeti na redio binafsi zilizofungiwa na kuwaruhusu wanadiplomasia wa kigeni kuonana na wafungwa ni miongoni mwa matakwa 17 ya Umoja wa Ulaya kwa serikali ya Jammeh.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO