Rwanda imepinga hatua ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani katika uchunguzi mashariki ya Congo kama ilivyopendekezwa na umoja wa mataifa hadi pale patakapokuwa na tathmini kamili ya matumizi yake, ikisema kuwa haitapenda Afrika kuwa sehemu ya majaribio kwa ajili ya upelelezi wa kutumia vyombo vya mataifa ya nje. Wajumbe wamesema kuwa mkuu wa ulinzi wa amani wa Umoja wa Mataifa Herve Ladsous ameliambia baraza la usalama jana katika kikao cha faragha kuwa ujumbe wa umoja wa mataifa katika jamhuri ya kidemokrasi ya Congo unapanga kutumia ndege tatu ambazo hazina rubani , katika jimbo la mashariki ya nchi hiyo lililokumbwa na mzozo.
Umoja wa mataifa ulihitaji ndege hizo zisizokuwa na rubani kwa ajili ya uchunguzi katika eneo la mashariki mwa Congo tangu mwaka 2008.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO