Saturday, January 12, 2013

SUDAN YAANGAMIZA WAASI 50 KORDOFAN KUSINI

Jeshi la taifa la Sudan  limefanikiwa kuwaangamiza waasi zaidi ya 50 na kuwajeruhi makumi ya wengine katika jimbo la Kordofan Kusini. Jeshi la Sudan limeeleza kuwa, mapigano hayo makali kati ya jeshi la serikali na kundi la waasi wa 'Harakati ya Mapinduzi' linaloundwa na makundi  manne ya waasi  yalijiri umbali wa kilomita 15 kutoka eneo la Kadugli, lililoko katikati mwa jimbo la Kordofan Kusini. Kabla ya hapo siku ya Jumanne iliyopita, Umoja wa Mataifa ulitahadharisha kuwa, mapigano yanayojiri katika jimbo la Kordofan Kusini yataleta athari mbaya kwa wananchi wa eneo hilo na maisha ya wananchi hao yatakuwa hatarini.
WAASI WA KORDOFAN

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO