Saturday, January 12, 2013

SAUDI NA ISRAEL WATEKELEZAJI WA NJAMA ZA MAREKANI


Kituo cha Kiutafiti na Kiistratijia cha Palestina kimetangaza kuwa, mashirikiano ya Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel yana lengo la kutekeleza malengo machafu ya Marekani katika eneo la Mashariki ya Kati. Taarifa iliyotolewa na kituo hicho imeeleza kuwa, mashirikiano ya Saudi Arabia na utawala wa Kizayuni wa Israel yamezidi kuongezeka katika miaka ya hivi karibuni, kwa kadri kwamba yameanzishwa mashirikiano ya siri ya pande mbili yenye lengo la kuanzishwa muungano mkubwa zaidi wa nchi za Kiarabu za Ghuba ya Uajemi na utawala wa Israel.
Ripoti ya Kituo cha Kiutafiti na Kiistratijia cha Palestina imeeleza kuwa, utawala wa Israel, tawala wa kifalme za nchi za Kiarabu za eneo la Ghuba ya Uajemi, Marekani na Jumuiya ya Kijeshi ya NATO zimeunda muungano utakaokuwa dhidi ya Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na nchi zinazoshirikiana na Iran katika eneo la Mashariki ya Kati na kusisitiza kwamba muungano huo umeundwa na Washington kwa lengo la kuvuruga amani na uthabiti katika eneo.

Ripoti hiyo imefichua kuwa, hitilafu za  kidini kati ya Waislamu na Wakristo na hali kadhalika kuweka mpasuko na hitilafu kati ya Masuni  na Mashia ni miongoni mwa malengo machafu ya muungano huo wa Saudi Arabia na utawala wa Israel. Taarifa ya kituo hicho imebainisha kuwa, fitna na uchochezi huo vinafanywa kwa shabaha ya kuendelea kubaki tawala za kifalme zilizopo katika eneo la Ghuba ya Uajemi na utawala wa Israel. Taarifa hiyo imesisitiza kuwa, Saudi Arabia na utawala wa Israel ndizo zinazokoleza hitilafu kati ya harakati za Kipalestina za  Fath na Hamas, na kuongeza kwamba,  zinafanya pia njama za kuitokomeza kabisa harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Hizbullah ya nchini Lebanon.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO