Saturday, January 12, 2013

THAILAND KUWAREJESHA WAISLAM KUTOA MYANMAR

Viongozi wa Thailand wamesema kuwa itawarudisha nchini Myanmar zaidi ya Waislamu 700 wa jamii ya Rohingya ambao waliokolewa hivi karibuni kutoka mikononi  kwa genge la wafanya magendo ya binadamu kusini mwa Thailand. Makundi ya kutetea haki za binadamu yameikosoa vikali serikali ya Thailand iliyopinga kufanya uchunguzi wa kina juu ya watu hao ambao wanakabiliwa na vitendo vya ukandamizaji na utesaji nchini mwao. 
Makundi hayo yameeleza kuwa, kulikuwa na  uwezekano mkubwa kwa Waislamu hao kupewa hifadhi kama wakimbizi kwa vile wanakimbia unyanyasaji na ukandamizaji unaofanywa na Mabudha wenye misimamo mikali  dhidi yao. Waislamu wa jamii ya Rohingya ambao ni wachache nchini Myanmar wanakandamizwa na Mabudha walio wengi nchini humo na wananyimwa haki wanazopewa wananchi wengine. Mapigano yaliyotokea  mwezi Juni mwaka jana kati ya Mabudha wenye misimamo ya kufurutu mipaka  dhidi ya Waislamu wa Rohingya katika jimbo la Rakhine, yalipelekea zaidi ya Waislamu 180  kuuawa na wengine zaidi ya laki  sita kuwa wakimbizi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO