Saturday, January 12, 2013

UINGEREZA IKIJIIONDOA EU ITATENGWA


Mwenyekiti wa kamati inayoshughulikia masuala ya Umoja wa Ulaya katika Bunge la Ujerumani amemtahadharisha Waziri Mkuu wa Uingereza, David Cameron akisema kuwa endapo London itajiondoa kwenye umoja huo itajikuta pabaya. Gunther Krichbaum amesema Uingereza itatengwa barani Ulaya iwapo itaandaa kura ya maoni kuamua iwapo ijiondoe au ibakie kwenye EU.
David Cameron amekuwa akiashiria kwamba huenda Uingereza ikajiondoa kwenye Umoja wa Ulaya kufuatia matatizo ya kiuchumi yanayozikumba nchi wanachama kwa sasa. Mwezi uliopita, Waziri wa Fedha wa Ujerumani, Wolfgang Schauble aliitaka London kukoma kutoa vitisho vya kujiondoa kwenye umoja huo na kumwambia Waziri Mkuu wa Uingereza kuwa, akiiondoa nchi yake kwenye Umoja wa Ulaya atajutia hatua hiyo milele.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO