Saturday, January 12, 2013

WANAJESHI WA UFARANSA WAINGIA MALI KWA SIRI


Habari kutoka kaskazini mwa Mali zinasema kuwa tayari wanajeshi wa Ufaransa wameingia kinyemela katika eneo hilo ili kuwasaidia wanajeshi wa serikali kukabiliana na waasi wa Ansaru Din ambao hapo jana walifanikiwa kuuteka mji muhimu wa Konna.
Rais Francois Hollande wa Ufaransa alisema hapo jana kwamba, nchi yake itakubali ombi lililotolewa na serikali ya Mali la kutuma jeshi kaskazini mwa nchi hiyo lakini duru za habari zinaarifu kuwa jeshi la Ufaransa liliingia Mali tangu usiku wa Jumatano. Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limeitaka Jumuiya ya Kiuchumi ya Nchi za Magharibi mwa Afrika (ECOWAS) kutuma mara moja kikosi chake kaskazini mwa Mali kabla waasi hawajateka miji zaidi ya nchi hiyo. Waasi wa Ansaru Din wameapa kukabiliana vikali na vikosi vyovyote vya kigeni vitakavyoingia Mali.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO