Tuesday, January 15, 2013

MAREKANI YASHIRIKI OPERESHENI YA SOMALIA

Marekani imesema kuwa wanajeshi wake walishiriki katika oparesheni iliyoshindwa ya kumkomboa afisa ujasusi wa Ufaransa aliyekuwa ametekwa nyara huko Somalia. Wanamgambo wa kundi la al Shabab wa Somalia Ijumaa usiku walimuua komandoo wa Ufaransa katika oparesheni iliyofeli ya kumkomboa Denis Allex afisa ujasusi wa Ufaransa aliyekuwa ametekwa nyara huko Somalia yapata miaka mitatu na nusu iliyopita. Wizara ya Ulinzi ya Ufaransa imetangaza kuwa komandoo mwingine wa nchi hiyo hajulikani alipo hadi hivi sasa. Rais Barack Obama wa Marekani alisema jana katika barua aliyoituma kwa Congress ya nchi hiyo kuwa wanajeshi wa Marekani walitoa kiwango fulani cha msaada wa kiufundi kwa vikosi vya Ufaransa katika oparesheni hiyo, na kwamba hawakuwa na nafasi ya moja kwa moja katika kulishambulia eneo hilo ambalo lililikuwa likisadikiwa kuwa ndipo alipokuwa akishikiliwa mateka afisa huyo wa ujasusi wa Ufaransa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO