Jeshi la Nigeria limemtia mbaroni Muhammad Zangina mmoja wa viongozi wa kundi
la Boko Haram. Taarifa ya jeshi la Nigeria imesema, Zangina ametiwa mbaroni
karibu na mji wa Maiduguri. Jeshi la Nigeria limesema kuwa, Zangina anatuhumiwa
kuhusika ana mashambulio kadhaa ya kigaidi dhidi ya raia na vikosi vya polisi
katika mji wa Maiduguri na kwamba, ametiwa mbaroni masaa machache kabla ya
kutekeleza mpango wa mashambulio mengine katika mji huo. itakumbukwa kuwa,
serikali ya Nigeria ilikuwa imetenga kitita cha dola laki moja na sitini elfu
kama zawadi kwa atakayetoa taarifa za uhakika za kutiwa mbaroni Muhammad
Zangina. Kundi la Boko Haram linatuhumiwa kuhusika na mauaji mengi yaliyofanyika
nchini Nigeria, na wanachama wake wamekuwa wakisakwa kwa udi na uvumba na jeshi
la nchi hiyo. Hadi sasa mamia ya watu wameshapoteza maisha yao na majengo kadhaa
ya serikali na makanisa kuchomwa moto kutokana na mashambulio yanayofanywa na
kundi hilo kaskazini mwa Nigeria.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO