Wabunge kadhaa nchini Uhispania wameikosoa vikali serikali ya nchi hiyo kwa
kupiga marufuku matangazo ya kanali za Televisheni za Press TV na Hispan TV
kutokana na mashinikizo ya lobi za Kizayuni na Marekani. Katika barua yao,
wabunge wa chama cha United Left wameitaka serikali ya Uhispania kutoa maelezo
iwapo Waziri wa Mambo ya Nje wa Uhispania Jose Manuel Garcia-Margallo alijadili
suala la kupiga marufuku kanali za Iran wakati alipokutana na lobi za Kizayuni
Oktoba mwaka 2012. Wabunge hao wamesema mmiliki wa shirika la satalaiti ya
Eutelsat ana uraia wa Israel na kwamba amekuwa akiongoza njama dhidi ya vyombo
vya habari vya Iran barani Ulaya.
Televisheni ya Iran ya Hispan TV hurusha
matangazo kwa lugha ya Kihispania kwa masaa 24 nayo Press TV hurusha matangazo
yake kwa lugha ya Kiingereza. Hivi karibuni televisheni za kimataifa za Iran
Hispan TV pamoja na Press TV zilipigwa marufuku kurusha matangazo yao kupitia
satalaiti za Ulaya za Eutelsat na Hotbird. Aidha Shirika la Intelsat limepiga
marufuku matangazo ya radio na televisheni kadhaa za kimataifa za Iran kufuatia
mashinikizo ya Umoja wa Ulaya. Maamuzi hayo ya kupiga marufu vyombo vya habari
vya Iran ni ishara ya wazi ya undumakuwili wa nchi za Magharibi zinazodai
kutetea uhuru wa maoni. Nchi za Ulaya na Marekani zikishirikiana na utawala wa
Kizayuni wa Israel zinajaribu kuzima sauti ya haki ya vyombo vya habari vya
Iran.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO