Waasi wa Somalia wa al Shabab wameitaka Kenya kuwaachilia huru Waislamu wote
wanaoshikiliwa kwa tuhuma za ugaidi na kutishia kuwa takwa hilo lisipotekelezwa
watawaua mateka wote wa Kenya wanaowashikilia. Waasi hao wametuma kwenye mtandao wa Tweeter video ya Wakenya wawili
waliowateka nyara katika kaunti ya Wajir mwaka uliopita na kuiambia serikali ya
Kenya kwamba maisha yao yapo hatarini.
Wiki iliyopita waasi wa al Shabab wa Somalia walisema kwamba wamemuua Denis
Allex, jasusi wa Ufaransa waliokuwa wanamshikilia mateka, ili kulipiza kisasi
kutokana na kile walichoeleza kuwa ni uadui wa Ufaransa kwa Waislamu na
mashambulizi yake ya kijeshi nchini Mali. Kenya inawashikilia watu kadhaa wanaodaiwa kuwa na uhusiano na kundi la as
Shabab na kuhusika katika mashambulizi ya kigaidi nchini humo.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO