Afisa mmoja wa Iran ameuawa nchini Syria. Tukio hilo la usiku wa kuamkia leo lilitokea wakati afisa huyo, Hesham Khoshnevis, alipokuwa akisafiri kutoka Damascus kwenda Lebanon. Taarifa ya ubalozi wa Iran mjini Beirut ilisema Khoshnevis, aliyekuwa na jukumu la kusimamia kamati ya ujenzi mpya wa Lebanon, aliuawa na wale uliowaita "Magaidi waliokuwa na silaha." Kamati hiyo iliundwa kutokana na uharibifu mkubwa uliofanywa na vita vya 2006 kati ya Israel na wanamgambo wa Kishia wa Hezbollah nchini Lebanon, ambao wanaungwa mkono na Iran. Hata hivyo taarifa ya ubalozi huo haikutaja jinsi afisa huyo wa Iran alivyouawa wala sehemu ya tukio.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO