Thursday, February 14, 2013

JASUSI MKUU WA ITALIA AFUNGWA MIAKA 10 JELA

Mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Kijeshi la Italia Niccolo Pollari amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela kwa kuhusika katika kumteka nyara Sheikh Osama Mustafa Hassan Nasr ‘Abu Umar’, Imam wa msikiti mmoja mjini Milan na kumpeleka nchini Misri mwaka 2003.
Mawakili wa Niccolo Pollari wamelalamikia hukumu hiyo na kusisitiza kwamba watakata rufaa kwenye Mahakama Kuu ya Italia. Marco Mancini msaidizi wa mkuu wa zamani wa Shirika la Ujasusi la Kijeshi la Italia alihukumiwa kifungo cha miaka 9 jela na wafanyakazi wengine watatu wa taasisi hiyo nao pia walihukumiwa vifungo vya miaka 6 kila mmoja.
Inafaa kuashiria hapa kuwa, Sheikh Osama Mustafa Hassan Nasr ‘Abu Umar’ mwanachuoni wa Kimisri ambaye alikuwa Imam katika msikiti mmoja mjini Milan, alitekwa nyara na kupelekwa nchini Misri mwaka 2003 kwa amri ya viongozi wa Shirika la Ujasusi la Marekani CIA kwa kisingizo cha kupambana na vitendo vya ugaidi.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO