Seneta wa zamani nchini Marekani John Kerry ameapishwa kushika nafasi ya Waziri wa Mambo ya Nje wa taifa hilo kubwa duniani. Kerry anachukua nafasi iliyoachwa wazi na waziri aliyemaliza muda wake Hillary Rodham Clinton ambaye aliitumikia wizara hiyo katika utawala wa muhula wa kwanza wa miaka minne wa Rais Barack Obama. Siku ya mwisho ya Clinton katika wadhifa huo ilimalizika kwa mashambulizi dhidi ya ubalozi wa nchi hiyo kwenye mji mkuu wa Uturuki, Ankara. Mripuaji pamoja na mlinzi wa ubalozi huo raia wa Uturuki wote waliuawa. Taasisi za kidiplomasia za Marekani nchini Uturuki zimekuwa zikilengwa mara kwa mara na makundi ya kigaidi. Mwaka 2008, shambulizi lililofanywa nje ya Ubalozi mdogo wa Marekani mjini Instanbul liliuwa askari polisi watatu pamoja na washambuliaji watatu. Shambulio hilo linaelezwa kufanywa na wanamgambo wenye mafungamano na kundi la al-Qaeda.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO