Kiongozi wa ngazi za juu wa Kanisa Katoliki nchini Uingereza ametangaza kujiuzulu wadhifa wake huo. Taarifa kutoka Vatican zinasema kuwa, Papa Benedict wa 16 Kiongozi wa Wakatoliki Duniani amekubali takwa la kujiuzulu Kadinali Keith O'Brien, Kiongozi wa Kanisa Katoliki la Uingereza. Kadinali O'Brien anasakamwa kwa kushindwa kuwachukulia hatua Mapadri waliokuwa chini yake ambao walikabiliwa na kashfa za kuwanajisi wafuasi wao. Kwa kujiuzulu Kadinali O'Brien Uingereza na Scotland hazitapata fursa ya kushiriki zoezi la kumchagua Papa mpya. Papa Benedict wa 16 atajiengua rasmi kutoka kwenye wadhifa huo tarehe 28 Februari mwaka huu.
Kadinali O'Brien alikuwa rafiki mkubwa wa mwandishi wa BBC aliyekuwa mashuhuri kwa kuwanajisi watoto wadogo kwa miaka mingi Jimmy Savile na inasemekana kuwa alimtukuza na mkumsifu mhalifu huyo baada ya kufariki dunia.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO