Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran limefanyia majaribio makombora matatu mapya. Naibu Kamanda wa kikosi hicho Kiumars Heidari amesema makombora hayo yaliyotengenezwa katika viwanda vya kijeshi hapa Iran yalifanyiwa majaribio yaliyofanya katika mazoezi ya hivi karibuni ya kikosi cha nchi kavu. Kamanda huyo amebainisha kuwa makombora hayo ni ya ardhi kwa ardhi.
Heidari ameongeza kuwa Kikosi cha Nchi Kavu cha Jeshi Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kitazindua magari mapya ya deraya Aprili 18 kwa mnasaba wa Siku ya Jeshi la Iran. Kamanda huyo ameashiria vitisho vya maaduui dhidi ya Iran na kuonya kuwa Iran itatoa pigo kubwa kwa adui yeyote atakayethubutu kuanzisha uchokozi. Wakati huo huo kamanda wa Jeshi la Wanamaji la Jamhuri ya Kiislamu ya Iran Admeli Habibullah Sayyari amesema mwezi ujao Iran itazindua meli mpya ya kivita.
Mwezi uliopita Iran ilizindua meli mpya ya kivita ijulikanayo kama Jamaran 2 itakayohudumu katika Bahari ya Kaspi. Manowari hizo za kisasa kabisa za zimetengenezwa kikamilifu hapa Iran kwa kutegemea wahandisi na wataalamu Wairani pasina msaada wa kigeni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO