Saturday, February 02, 2013

LEBANON YAZITAKA NCHI ZA KIARABU KUCHUKUA HATUA DHIDI YA HUJUMA ZA ISRAEL SYRIA

Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Lebanon, amezitaka nchi za Kiarabu kuchukua msimamo imara na madhubuti kuhusiana na mashambulio ya anga yaliyofanywa na ndege za utawala katili wa Kizayuni nchini Syria. Adenan Mansur ameyasema hayo hii leo katika radiamali ya kulaani vikali mashambulizi ya jioni ya jana ya utawala wa Kizayuni dhidi ya kituo cha utafiti wa sayansi cha Jamraya karibu na mji mkuu Damascus ambapo wafanyakazi wawili wa kituo hicho waliuawa na wengine watano kujeruhiwa. Amesema kuwa, nchi za Kiarabu zinatakiwa kuchukua msimamo imara dhidi ya hujuma hizo na kwamba, suala hilo ni la lazima. Mansur pia amesema, kwa mara kadhaa utawala haramu wa Kizayuni umekuwa ukitishia amani na usalama wa nchi za Kiarabu na kwamba, shambulio la Israel nchini Syria kwa mara nyingine linadhihirisha zaidi jinai na ukatili wa utawala huo haramu tangu ulipoasisiwa mnamo mwaka 1948 hadi leo. Tayari Wizara ya Mambo ya Nje ya Russia imetoa ripoti na kusema kuwa, iwapo habari hizo zitakuwa na ukweli basi hilo litahesabiwa kuwa ni shambulio la kichokozi dhidi ya nchi huru jambo ambalo linakiuka Hati ya Umoja wa Mataifa.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO