Saturday, February 02, 2013

WAMAGHARIBI HAWATAKI KUUTATUA MGOGORO WA SYRIA


Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Russia amesema kuwa, nchi za Magharibi zikiongozwa na Marekani zinazuia juhudi za Moscow za kuutatua mgogoro wa Syria kwa mujibu wa makubaliano ya Geneva. Alexander Lukashevich amesema kuwa, baadhi ya mikakati ya Russia yenye lengo la kukomesha mgogoro wa Syria imekuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa wa nchi za Magharibi na hasa Marekani.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje wa Russia ameongeza kuwa, Moscow inaamini kwamba kipindi hiki kinahitaji kuchukuliwa hatua madhubuti na za haraka zenye shabaha ya kukomesha machafuko nchini Syria, kwa kufunguliwa milango ya kufanyika mazungumzo. Lukashevich amesema kuwa, mgogoro wa Syria kamwe hauwezi kutatuliwa kwa njia ya mtutu wa bunduki.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO