Wednesday, February 13, 2013

MAADUI HAWAWEZI KUKABIIANA NA IRAN


Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu Ayatullah Ali Khamenei amesema kuwa, maadui wametambua kwamba hawawezi kukabiliana na taifa la Iran. Ayatullah Ali Khamenei amesema hayo leo ambapo pia amepongeza kujitokeza kwa wingi wananchi wa Iran katika maandamano ya nchi nzima hapo jana kwa mnasaba wa kuadhimisha mwaka wa 34 tangu ushindi wa Mapinduzi ya Kiislamu yaliyohitimisha utawala wa kifalme uliokuwa ukiungwa mkono na Marekani. Kiongozi Muadhamu amesema, mara zote ambapo adui anayepinga uhuru na utukufu wa taifa la Iran anapotaraji kuwa wananchi hawataitikia wito wa Mapinduzi na Jamhuri ya Kiislamu, wananchi wa Iran humkatisha tamaa kwa mahudhurio yao makubwa.
Hapo jana mamilioni ya wananchi wa Iran walijitokeza katika mji mkuu Tehran na katika miji mingine nchini, kuonyesha kwa mara nyingine uungaji mkono wao kwa mfumo wa Jamhuri ya Kiislamu ulioasisiwa na Hayati Imam Khomeini (M.A).

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO