Wednesday, February 13, 2013

ISRAEL YAJENGA ZAIDI UKINGO WA MAGHARIBI


Licha ya kukosolewa kimataifa kutokana na ujenzi wake wa vitongoji vya walowezi wa Kizayuni katika ardhi za Palestina unazozikalia kwa mabavu, Israel imetangaza mpango wa kujenga nyumba 90 zaidi katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan. Mpango huo umepitishwa leo na kamati ya mipango ya utawala wa kiraia na ujenzi wa vitongoji hivyo vya walowezi utaanza baada ya wiki kadhaa. Kwa mujibu wa Umoja wa Mataifa ujenzi huo wa Israel si halali kwa sababu Tel Aviv iliyakalia kwa mabavu maeneo hayo ya Palestina katika vita vya mwaka 1967 na suala hilo linakinzana na makubaliano ya Geneva yanayopiga marufuku ujenzi katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
Kwa upande mwingine Sami Abu Zuhr, Msemaji wa Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) amesema kuwa, Marekani inakwamisha mwenendo wa utekelezwaji makubaliano ya maridhiano ya kitaifa la Palestina.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO