Mawaziri wa Ufaransa wanakutana katika kikao cha
dharura kuzungumzia kugundulika kwa uuzwaji wa nyama ya farasi katika viwanda
vya nyama nchini humo. Hali hii imezua maswali mengi kuhusu umakini wa
viwanda vya nyama vinavyofanya biashara hiyo na kuthibitisha ubora wa nyama
barani humo huku mataifa yanayoathiriwa yakiwa pia ni Uingereza,
Ufaransa, Sweden , Ireland na Romania.Inahofiwa kuwa mataifa mengine 11 huenda
yakaathiriwa na uingizwaji na uuzwaji wa nyama hiyo ikiwa hatua madhubuti
hazitachukuliwa. Waziri anayehusika na maswala ya vyakula nchini Ufaransa
Guillaume Garot amesema kuwa lengo lake ni kuondoa nyama hiyo kwenye maduka
yote nchini humo.
Wamiliki wa maduka makubwa nchini Ufaransa wameondoa bidhaa
zenye nyama kwa hofu hiyo huku idadi ya wateja nayo ikipungua. Mwezi uliopita,
wakaguzi wa chakula nchini Ireland walitangaza kuwa walipata nyama ya farasi
katika bidhaa mbalimbali katika maduka makubwa nchini humo. Madkatari
wanaonya kuwa nyama hiyo inaweza kuwa na madhara kwa binadamu kwa sababu ya
chanjo inayotumiwa kuwachanja farasi hao.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO