Papa Benedict wa 16 amejiuzulu rasmi hii leo baada ya kuliongoza Kanisa Katoliki kwa miaka 8. Papa mwenye umri wa miaka 85 amesema umri na afya yake haviwezi kumruhusu kutekeleza majukumu yake ingawa weledi wa mambo wamedai kwamba, kashfa za ngono dhidi ya makasisi wa ngazi za juu mjini Vatican na juhudi za Papa za kufunika uozo huo ni miongoni mwa sababu za kujiuzulu kwake. Benedict wa 16 alichukua hatamu za uongozi wa Kanisa Katoliki mwezi Aprili mwaka 2005 kufuatia kufariki dunia Papa wa wakati huo, John Paul II. Papa Benedict wa XIV ameahidi kutoingilia uendeshaji wa Vatican na kwamba atamuheshimu na kumuunga mkono Papa mpya atakayechaguliwa. Mara ya mwisho kwa Papa wa Kanisa Katoliki kujiuzulu ilikuwa ni miaka 600 iliyopita.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO