Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran amesema serikali inatathmini kwa kina njama za kiuchumi za maadui ili kuzisambaratisha. Akizungumza jana usiku na wananchi kwa njia ya moja kwa moja katika Kanali ya Kwanza ya Televhisheni ya Kitaifa ya Iran, Rais Ahmadinejad amesema baada ya kuchunguza kwa kina njama za maadui serikali imetayarisha bajeti yenye ubunifu mkubwa. Amesema kwa mujibu wa bajeti ya mwaka mpya wa Kiirani wa 1392, unaoanza Machi 21, uchumi wa Iran utarejea katika hali ya kawaida na hivyo kufelisha njama za maadui. Amesema bajeti mpya ya Iran imepunguza utegemezi kwa pato la mafuta. Akiashiria vikwazo vya nchi za Magharibi dhidi ya Iran, rais Ahmadinejad ametoa wito kwa watu wote Iran kushirikiana ili nchi iweze kupita vizuri katika kipindi hiki. Amesema Iran ni nchi yenye uwezo mkubwa na kuongeza kuwa pamoja na kuwa maadui na hasa serikali ya Marekani inatumia uwezo wake wote kuishinikiza Iran lakini haitafanikiwa katika malengo yake hayo. Amesema Wamarekani walidhani kwa pigo la kiuchumi kwa Iran, nchi hii ingeyumba lakini, Alhamdulillah, Iran imesimama imara.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO