Shirika moja la Russia linalouza silaha kimataifa limesema limetuma shehena
ya silaha nchini Mali na kwamba limepanga kutuma silaha zaidi katika nchi hiyo
Kiafrika iliyotumbukia kwenye vita vinavyoongozwa na Ufaransa.
Anatoly Isaikin Mkurugenzi wa Shirika la Rosobornexpo amesema shehena ya
kwanza ilitumwa wiki mbili zilizopita na mazungumzo yanaendelea kutuma shehena
zingine ndogo ndogo. Ufaransa ilianzisha vita nchini Mali Januari 11 kwa
kisingizio cha kupambana na waasi wa kaskazini mwa nchi hiyo. Nchi za Umoja wa
Ulaya pamoja na Marekani zinaunga mkono hujuma hiyo inayoongozwa na Ufaransa
nchini Mali.
Maelfu ya raia wa nchi hiyo ya Magharibi mwa Afrika wamelazimika kukimbia na
kuyahama makazi yao baada ya vikosi vinavyoongozwa na Ufaransa kuingia eneo la
kaskazini mwa nchi hiyo.
Weledi wa mambo wanaamini kuwa lengo kuu la Ufaransa katika vita vya Mali si
kupambana na waasi bali ni kupora utajiri wa nchi hiyo kama vile mafuta ya
petroli, dhahabu na madini ya urani.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO