Maafisa wa Umoja wa Mataifa wameelezea wasiwasi wao kuhusiana na hali mbaya
ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel, hasa juu ya
hali ya kiafya ya Samer Issawi anayegoma kula.
Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa na Umoja wa Mataifa, James Rawley Mratibu wa
Masuala ya Kibinadamu wa Umoja wa Mataifa katika ardhi za Palestina zinazokaliwa
kwa mabavu alikutana na Issa Qaraqe, Waziri wa Mamalaka ya Ndani
anayeshughulikia masuala ya wafungwa wa Palestina katika Ukingo wa Magharibi wa
Mto Jordan. Katika mazungumzo yao Rawley alisema kwamba Umoja wa Mataifa una
wasiwasi mkubwa juu ya Wapalestina wanaoshikiliwa katika jela za Israel.
Wakati huo huo Eduardo Del Buey Naibu msemajiwa wa Ban Ki Moon Katibu Mkuu wa
Umoja wa Mataifa amesema kuwa, wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa katika
jela za Israel bila kufunguliwa mashtaka wanapaswa kuhukumiwa au kuachiliwa
huru. Wapalestina 4,610 wanashikiliwa katika jela za kuogofya za Israel kutokana
na sababu za kisiasa.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO