Bomba la mafuta toka Misri hadi Israel |
Waziri wa Mafuta wa Misri amesema Cairo itaushurutisha utawala haramu wa
Israel kulipa gharama za utajiri wa Misri iliyoupora. Waziri wa Mafuta wa Misri
Osama Kamal amenukuliwa akisema kuwa wakati utawala wa Kizayuni wa Israel
ulipokalia kwa mabavu eneo la Sinai kuanzia mwaka 1976 hadi 1977, ulipora
utajiri wa petrokemikali katika eneo hilo. Kwa mujibu wa wataalamu,
petrokemikali yenye thamani ya dola bilioni 480 iliporwa na Israel katika eneo
hilo. Kamal amesema Misri inapanga mkakati wa kuhakikisha kuwa utawala wa
Kizayuni unashurutishwa kulipa dola bilioni 500 kama fidia ya utajiri huo.
Ameongeza kuwa hivi sasa Misri imebatilisha mikataba ya kuiuzia Israel gesi
asilia. Katika zama za dikteta wa Misri Hosni Mubarak aliyetimuliwa madarakani,
Misri ilikuwa ikiizuia Israel gesi asilia kwa bei ya chini sana na hivyo
kuwasababishia Wamisri hasara kubwa. Lakini baada ya mapinduzi ya wananchi wa
Misri, nchi hiyo ilisitisha upelekaji gesi kwa utawala wa Kizayuni.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO