Monday, March 11, 2013

ALQAEDA YAWAUWA WANAJESHI 48 WA SYRIA

Kundi la mtandao wa Al-Qaida limedai kuhusika na mauaji ya wanajeshi 48 wa Syria pamoja na walinzi 9 wa Iraq  huko magharibi mwa Iraq wiki iliyopita. Kwa mujibu kwa kundi la kijasusi lenye makao yake Marekani linaloitwa SITE ambalo linafuatilia mikutano ya mtandao huo wa al-Qaida limesema kwamba wanamgambo hao wametoa taarifa katika tovuti yao hii leo wakidai kuhusika na mashambulizi ya wiki iliyopita. Wanajeshi wa Syria walikuwa wamekimbilia kaskazini mwa Iraq wakati wa mapambano ya hivi karibuni na walikuwa wakisindikizwa kurudi Syria kupitia mpaka wa Iraq kwenye mkoa wa Anbar wakati waliposhambuliwa. Tukio hilo lilionyesha kwamba kuna uwezekano wa kuwepo ushirikiano wa karibu kati ya tawi la al-Qaida nchini Iraq na washirika wake wenye itikadi kali ndani ya Syria ambao wanapigana upande wa waasi katika mgogoro wa Syria.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO