Helikopta ya Umoja wa Mataifa imeanguka mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na kuuwa watu wote waliokuweko kwenye helikopta hiyo. Hayo yamesemwa na msemaji wa masuala ya kijeshi wa Umoja wa Mataifa. Kanali Prosper Basse amesema helikopta hiyo ilianguka jana katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini. Duru za habari za Magharibi zimeripoti kuwa helikopta hiyo ya Umoja wa Mataifa ilianguka umbali wa kilomita 35 kutoka Bukavu makao makuu ya mkoa huo. Basse amesema kuwa watu waliokuwemo katika helikopta hiyo wote walikuwa ni Warussia na kwamba helikopta hiyo ilikuwa ikirejea Bukavu baada ya shughuli zake huko magharibi mwa mkoa wa Kivu ya kaskazini. Tarehe 5 mwezi Machi mwaka huu ndege nyingine ilianguka katikati mwa mji wa Goma na kuuwa watu sana na kuwajeruhi wengine watatu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO