Rais Asif Ali Zardari wa Pakistan anaelekea Iran hii leo kuhudhuria sherehe maalum za ufunguzi wa ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Iran kwenda Pakistan, mradi ambao umezusha utata na kupingwa vikali na Marekani. Mradi huo kati ya mataifa hayo mawili ya Kiislamu umelenga kuwasaidia Wapakistan kukabiliana na ongezeko la mahitaji ya nishati katika wakati huu ambapo nchi hiyo inakabiliwa na uhaba wa nishati. Hata hivyo kuna wasiwasi mkubwa kuhusu ikiwa Pakistan itaweza kumudu gharama zinazohitajika katika kuukamilisha ujenzi huo na ikiwa itaweza kuendelea na mradi huo kabla ya kukabiliwa na vikwazo kutoka Marekani. Pakistan itahitajika kulipa dolla bilioni 1.5 kukamilisha mradi huo. Ziara hiyo ya Rais Zardari na ufunguzi wa mradi huo mpya inakuja siku kadhaa kabla ya muda wa serikali ya Pakistan madarakani kumalizika na hatua hiyo huenda imelengwa kukiimarisha chama tawala cha nchi hiyo PPP, kujipatia kura kwa kujionyesha kinalishughulikia suala la tatizo la nishati.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO