Tuesday, March 12, 2013

HAMAS YASISITIZA KUINGIZA SILAHA UKANDA WA GHAZA


Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina Hamas imesisitiza kuwa, serikali iliyochaguliwa na wananchi wa Palestina ina haki ya kuingiza silaha katika eneo la Ukanda wa Gaza.
Msemaji wa Hamas Sami Abu Zuhri amesema kuwa, si jinai kuingiza silaha Ukanda wa Gaza kwani silaha hizo zinatumiwa kwa shabaha ya kujihami na mashambulizi yanayofanywa na utawala wa Kizayuni wa Israel.
Abu Zuhri ameongeza kuwa, hakuna nchi yoyote ulimwenguni inayoweza kuzuia kuingizwa silaha katika eneo hilo. Msemaji wa Hamas ameongeza kuwa, inasikitisha kuona kuwa, licha ya wananchi wa Palestina kushambuliwa na silaha nzitonzito na za kisasa  za utawala wa Kizayuni wa Israel, jumuiya na taasisi za Kiarabu zimekuwa kimya na kukodoa  macho Wapalestina wakiendelea kuwekewa vikwazo, mzingiro na kushambuliwa kwa makombora ya Wazayuni.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO