Mufti Mkuu wa Syria ametangaza kuwa, serikali na taifa la Syria linakaribia kupata ushindi dhidi ya magaidi wanaendesha machafuko na kufanya mauaji dhidi ya watu wasio na hatia yoyote. Sheikh Ahmad Badruddin Hassoun amesisitiza kwamba, Syria inakabiliana vilivyo na magaidi na hivi sasa inaelekea kupata ushindi. Mufti Hassoun amebainisha kwamba, taifa la Syria sio taifa ambalo linakubali kunyongeshwa au kusalimu amri mbele ya dhulma na wala si taifa lenye kukubali kutwishwa mambo. Mufti Mkuu wa Syria amesisitiza kwamba, hivi sasa taifa hilo linalipa gharama ya kusimama kwake kidete dhidi ya siasa za kupenda kujitanua za utawala wa Kizayuni wa Israel na waitifaki wake. Sheikh Badruddin Hassoun ameashiria njama za maadui dhidi ya serikali ya kimuqawama ya nchi hiyo na kusisitiza kwamba, maadui wakiwa na lengo la kutoa pigo kwa muqawama wameanzisha njama kubwa dhidi ya serikali na taifa la Syria; lakini taifa hili litasambaratisha njama zote za maadui na kupata ushindi.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO