Tuesday, March 12, 2013

MAREKANI YAITISHA PAKISTAN JUU YA BOMBA LA GESI TOKA IRAN


Baada ya kuzinduliwa rasmi awamu ya kwanza ya ujenzi wa bomba la kusafirisha gesi kutoka Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hadi Pakistan, serikali ya Marekani imeingilia kati na kutoa vitisho vya kuiwekea vikwazo Pakistan kwa vile imeshirikiana na Iran kwenye mradi huo.
Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Marekani Victoria Nuland amesema kuwa, Washington imeingiwa na wasiwasi juu ya ujenzi wa bomba hilo la kusafirisha gesi kutoka Iran hadi Pakistan. Jana Jumatatu, Marais wa Iran na Pakistan walizindua mradi wa ujenzi wa bomba la gesi utakaogharimu kiasi cha dola bilioni 7.5, licha ya mashinikizo makubwa yanayotolewa na  Marekani. Rais Mahmoud Ahmadinejad wa Iran alisema kwenye uzinduzi huo kwamba nchi za Magharibi hazina haki ya kuzuia mradi huo. Imekadiriwa kuwa ujenzi wa bomba hilo lenye urefu wa kilomita 1,600 utachukua muda wa miaka miwili.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO