Saturday, March 02, 2013

IRAN INA UWEZO WA KUJIBU MAPIGO YOYOTE


Naibu kamanda wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran (SEPAH) Brigedia Jenerali Hussein Salami amesema kuwa Iran ina uwezo wa kujibu mashambulizi ya nchi yoyote. Salami ameashiria mafanikio makubwa ya Iran katika utengenezaji wa zana mbalimbali za kujihami na kusema taifa la Iran litajibu mapigo ya dola lolote lile kwa kutumia nguvu ya imani na uwezo wake wa silaha za kijihami. 
Ameongeza kuwa baada ya kushindwa katika medani za kivita sasa adui analenga taifa la Iran katika medani za masuala ya kiutamaduni na kiuchumi. Amesisitiza kuwa licha ya njama hizo lakini Jamhuri ya Kiislamu imepata mafanikio makubwa katika nyanja mbalimbali za kisayansi na kielimu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO