Wednesday, March 20, 2013

IRAN YALAANI SILAHA ZA SUMU KUTUMIWA NA WAASI WA SYRIA


Iran imewalaani vikali waasi wanaopata himaya ya kigeni nchini Syria kwa kutimia silaha za sumu dhidi ya raia katika mji wa Halab kaskazini magharibi mwa nchi hiyo ambapo watu 25 wamepoteza maisha hadi sasa. Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran Ramin Mehmanparast amesema Jumatano kuwa, Tehran inalaani vikali kitendo hicho cha waasi kilicho dhidi ya ubinaadamu cha kutumia silaha za simu katika mji wa Halab.
Mehmanparas pia amekosoa vikali nchi zinazowaunga mkono waasi wa Syria na kusema nchi hizo zinabeba lawama ya jinai za waasi hao. Imearifiwa kuwa watu wasiopungua 25 wameuawa na wengine 86 kujeruhiwa baada ya waasi kufyatua makombora yenye gesi za sumu katika kijini cha Khan al-Assal mjini Halab (Aleppo). Wanawake na watoto ni kati ya wahanga wa jinai hiyo. Kati ya nchi zinazowaunga mkono waasi nchini Syria ni Marekani, Ufaransa, Qatar, Saudi Arabia na Uturuki.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO