Rais Barack Obama wa Marekani leo amewasili nchini Israel, na akawahakikishia Waisraeli kuwa Marekani imejitolea kikamilifu katika kuhakikisha usalama wa raia wa nchi hiyo. Akizungumza muda mfupi baada ya ndege yake kutua katika uwanja wa ndege wa Ben Gurion mjini Tel Aviv, Obama amesema wanasimama pamoja kwa sababu amani ni lazima ipatikane katika ardhi hiyo takatifu. Waziri Mkuu Benjamin Nentanyahu amedokeza kuwa haja ya kuwepo ushirikiano kati ya nchi hizo mbili ni kubwa sana kuliko jinsi ilivyokuwa awali, na ni muhimu katika kupatikana uimara na amani. Punde baada ya kutolewa hotuba za kumkaribisha, Obama aliutembelea mtambo wa Israel wa kujikinga dhidi ya makombora wa Iron Dome, ambao uliwekwa katika uwanja wa ndege kwa ajili ya ziara yake. Mtambo huo ulitengenezwa kwa ufadhili mkubwa wa Marekani, na hatua ya Ris wa Marekani kuutembelea mtambo huo imetajwa na Israel kuwa alama ya ushirikiano mkubwa wa kiusalama baina ya nchi hizo mbili chini ya utawala wa Obama.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO