Tuesday, March 12, 2013

KIBLA CHA KWANZA CHA WAISLAM KIKO HATARINI

Mkuu wa Idara ya Masuala ya Quds ametoa wito wa kukabiliana kwa nguvu zote na mpango wa Kizayuni wa kutaka kuugawa Msikiti Mtakatifu wa al-Aqswa. Ahmed Qurei amenukuliwa na Mtandao wa Habari wa Quds Net akisema kwamba, utawala wa Kizayuni wa Israel umejiandaa kutekeleza mpango wa kuigawa Masjdul Aqswa. Amesema, endapo Wapalestina hawatachukua hatua za maana za kukabiliana na mpango huu hatari, basi kutatokea matukio ya kuhuzunisha katika msikiti huo mtakatifu wenye hisotia kongwe. Mkuu wa Idara ya Masuala ya Quds amewataka Wapalestina kujitokeza kwa wingi katika msikiti huo hususan katika siku za Ijumaa kwa ajili ya Sala ya Ijumaa na kuongeza kuwa, moja ya njia za kukabiliana na mpango huo wa Wazayuni ni kwenda kwa wingi katika msikiti huo. Aidha Ahmed Qurei amewataka Waislamu kote ulimwenguni kuungana na Wapalestina katika kukabiliana na njama za utawala wa Kizayuni wa Israel za kutaka kuugawa msikiti wa al-Aqswa kibla cvha kwanza cha Waislamu.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO