Tuesday, March 12, 2013

IRAN WAIKIMBIZA NDEGE YA KIJASUSI YA MAREKANI ILIYOINGIA ANGA YAKE

Kamanda wa ngazi za juu wa kijeshi wa Iran amesema vikosi vya ulinzi nchini vimefanikiwa kuitambua na kuitimua ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya U2 ambayo ilikuwa inajaribu kuingia katika anga ya Iran kwenye eneo la Bahari ya Oman. Kamanda wa Kituo cha Ulinzi cha Khatam al-Anbiya, Brigedia Jenerali Farzad Esmaili amewaambia waandishi habari leo Jumanne kuwa, mnamo Februari 10 mwaka huu, mfumo wa ulinzi wa anga wa Iran ulifanikiwa kuigundua ndege hiyo ya kijasusi ambayo ina uwezo wa kukwepa rada. Amesema, ndege hiyo iliondoka haraka katika eneo hilo baada ya kupokea onyo kali kutoka kwa vikosi vya Iran vya ulinzi wa anga. Kamanda huyo ameongeza kuwa, ndege ya U2 ndio ndege ya kisasa kabisa ya kijasusi duniani na yamkini ilikuwa inakusudia kuchukua picha na kupata habari za kijasusi katike eneo la kusini mwa Iran. Katika miezi ya hivi karibuni vikosi vya ulinzi vya Iran vimefanikiwa kunasa ndege za kijasusi za Marekani. Ikumbukwe kuwa, Desemba 4 mwaka 2012, Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu SEPAH lilitangaza kuwa lilifanikiwa kunasa ndege ya kijasusi ya Marekani aina ya ScanEagle katika maji ya Ghuba ya Uajemi. Aidha Desemba mwaka 2011 Disemba 4 mwaka jana Iran ilitangaza kuwa kitengo chake cha masuala ya kielektoroniki katika vikosi vya jeshi kimefanikiwa kuidhibiti ndege hiyo ya kijasusi ya Marekani aina ya RQ-170 Sentinel ambayo ilikuwa ikipaa katika anga ya mji wa Kashmar huko kaskazini magharibi mwa Iran na baadae kuishusha chini baada ya kuisababishia kasoro ndogo sana.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO