Saturday, March 16, 2013

MAREKANI KUANZISHA MASHAMBULIZI YA DRONE SYRIA

Maafisa wa kitengo cha kupambana na ugaidi cha Marekani wamesema kuwa Shirika la Ujasusi la nchi hiyo (CIA) linafikiria kupanua mashambulizi ya ndege zisizo na rubani huko Syria.  Maafisa hao wamesema kuwa kitengo hicho kinachoendesha oparesheni za ndege za ujasusi huko Pakistan na Yemen hivi karibuni kimewaamuru baadhi ya majasusi wake kukusanya taarifa zaidi za kiitelijesnia kuhusu hali ya mambo huko Syria. Gazeti la los Angeles Time limeripoti kuwa maafisa hao wa Marekani wanaofanya kazi kwenye makao makuu ya CIA huko Langley wameasisi timu na kikosi kingine cha majasusi wa nchi hiyo walioko Iraq ili kuchunguza madai ya kuweko vitisho dhidi ya maslahi ya Marekani huko Syria. Los Angeles Times limeongeza kuwa timu hiyo inafanya kazi bega kwa bega na Saudi Arabia, Jordan na mashirika mengine ya ujasusi ya kieneo. 

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO