Saturday, March 16, 2013

POLISI KENYA YAPAMBANA NA WAFUASI WA ODINGA

Polisi mjini Nairobi imetumia gesi ya kutoa machozi, kuwatawanya wafuasi wa mgombea urais alieshindwa nchini Kenya Raila Odinga, waliokusanyika mbele ya mahakama ya juu kabisa leo, saa chache kabla ya mawakili wake kuwasilisha pingamizi juu ya kushindwa kwake. Mtu moja ameripotiwa kujeruhiwa wakati polisi ikiliondoa kundi hilo mbele ya jengo la mahakama. Akizungumza na wafuasi wa Odinga baada ya kuwasilisha pingamizi hilo, moja wa mawakili James Orengo ameielezea siku hii kuwa ni ya kihistoria. Baadhi ya wafuasi wa Odinga walivalia fulana zenye maandishi yanayounga mkono pingamizi, mengine yakisema demokrasia majaribuni, maneno ambayo yanarudia matamshi ya Odinga kuwa pingamizi lake litakuwa mtihani wa demokrasia nchini Kenya. Odinga alikataa kutambua ushindi mdogo wa Uhuru Kenyatta katika duru ya kwanza, na washirika wake wanasema muungano wake wa Jubili ulikula njama na tume ya uchaguzi kumpa ushindi. Kenyatta na tume hiyo wanakanusha kufanya njama zozote kuiba kura.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO