Tuesday, March 12, 2013

BUNGE LA ETHIOPIA KUJADILI MGAO WA MAJI YA MTO NILE


Serikali ya Ethiopia hivi karibuni itajadili kwenye bunge la nchi hiyo makubaliano ya 'Entebbe' juu ya kugawanywa kwa uadilifu maji ya Mto Nile. Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje ya Ethiopia imeeleza kuwa, makubaliano ya Entebbe ya kugawana maji ya Mto Nile yanapingwa vikali na nchi za Sudan na Misri ambazo zimekuwa zikistafidi mno na maji hayo katika kilimo cha umwagiliaji. Taarifa ya wizara hiyo imeeleza kuwa, mpango huo ulisimamishwa kwa sababu ya zoezi la uchaguzi wa rais na bunge nchini Misri. Taarifa hiyo imeongeza kuwa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo nayo tayari imeshatia saini makubaliano hayo na nchi ya Sudan Kusini pia imetangaza kuwa itayasaini hivi karibuni.
Makubaliano ya Entebbe yanataka kupunguza hisa ya nchi za Misri na Sudan na kuziongezea hisa nchi nyingine zinazochangia maji ya Mto Nile kwa njia ya usawa. Nchi 11 zinazochangia maji ya Mto Nile ni Uganda, Kenya, Tanzania, Rwanda, Misri, Sudan, Sudan Kusini, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Eritrea na Burundi. Inafaa kuashiria hapa kuwa, Ethiopia, Uganda, Tanzania, Rwanda, Kenya na Eritrea zilitangaza kwamba makubaliano ya mwaka 1929 hayakuwa ya kiadilifu, na hivyo ziliamua kutia saini makubaliano ya Entebbe ya mwezi Mei 2010 kwa lengo la kugawana kwa usawa matumizi ya maji ya Mto Nile.

No comments:

Post a Comment

TUPE MAWAZO YAKO