Chama tawala cha Kongresi ya Taifa Sudan
kimefichua kuwepo njama za mashirika ya kijasusi ya Marekani na Utawala wa
Kizayuni ya Israel za kuwaunga mkono waasi nchini Sudan lengo likiwa ni
kuyakalia kwa mabavu maeneo yenye utajiri wa mafuta nchini humo.
Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Fars,
chama hicho tawala nchini Sudan kimesema majasusi wa Israel na Marekani wanaunga
mkono makundi ya waasi hasa kundi la JEM la Darfur. Chama cha Kongresi ya Taifa
kimesema pamoja na kuwepo oparesheni hizo za majasusi wa Kizayuni na Marekani,
jeshi la Sudan liko macho na litaangamiza njama hizo kikamilifu. Aidha chama
hicho kimesema Umoja wa Mataifa umeshatoa ripoti inayoonyesha kuwa serikali ya
Sudan Kusini inawaunga mkono waasi wanaoipinga serikali ya Sudan. Hamid Sadiq wa
Kongresi ya Taifa amesema ripoti hiyo ya Umoja wa Mataifa imethibitisha ukweli
ambao Sudan imekuwa ikiusema mara kwa mara. Wiki iliyopita pia Qutbi al Mahdi
mmoja wa viongozi wa chama tawala cha Kongresi ya Taifa ya Sudan alifichua njama
za nchi za Magharibi za kutaka kuwalazimisha watu wa Sudan wawe Wakristo
sambamba na kuibua hitilafu za kikabila nchini humo lengo likuwa ni kuipokonya
nchi hiyo utambulisho wake asili.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO