Maafisa wa kitengo cha kusimamia na kukagua bidhaa nchini Norway wamegundua kuwepo kwa nyama ya nguruwe iliyochanganywa na nyama halali nchini humo. Catherine Signe Svinland Mshauri wa Kitengo cha kusimamia na kukagua bidhaa nchini Norway amesema kuwa, kimegunduliwa kiasi cha asilimia 5 hadi 30 ya nyama ya ngurume kwenye nyama ya ng'ombe ambayo imeandikwa kuwa halali kwenye maduka kadhaa nchini humo. Amesisitiza kuwa kiwango hicho cha nyama ya nguruwe hakikuwekwa kwa bahati mbaya kwenye nyama halali. Amesema kuwa, wakaguzi hao pia wamegundua kwenye sehemu inayouzwa Pizza kukiwa na nyama ya ng'ombe lakini imechanganywa kwa asilimia 60 na nyama ya nguruwe. Kwa upande mwengine, siku ya Alhamisi, maafisa wa ukaguzi nchini Uingereza waligundua masalio ya nyama ya nguruwe kwenye soseji ya kuku kwenye mkahawa ulioko kwenye shule moja mjini London. Inafaa kuashiria hapa kuwa, wiki chache zilizopita, kuliibuka kashfa kubwa ya uuzwaji na usambazwaji wa nyama ya farasi katika nchi mbalimbali za Ulaya. Imeelezwa kuwa, sababu ya kuuzwa nyama ya farasi badala ya ng'ombe katika nchi kadhaa za Ulaya, inatokana na urahisi wa bei ya nyama ya farasi. Amma kashfa hiyo imezusha mgogoro mkubwa wa kiafya, kwani duru za kitiba zinaeleza kwamba nyama ya farasi ina mada za sumu.
No comments:
Post a Comment
TUPE MAWAZO YAKO